Wanandoa wa Urusi walivyotoa habari za ujasusi kwa Ukraine

Wakati Sergei na Tatyana Voronkov walipohama kutoka Urusi kwenda kijiji kidogo cha Ukraine, walitarajia kuishi maisha ya utulivu, lakini mambo yaligeuka na kuwa tofauti sana na matarajio yao.
Baada ya uvamizi mkubwa wa Moscow, wenzi hao walijikuta katika eneo linalokaliwa na waliamua kuwa watoa habari za ujasu kwa jeshi la Ukraine.
Kilichofuata ni kuwekwa kizuizini, kuhojiwa, na kutoroka kwenda Ulaya kwa kutumia hati za uongo - na pete ya mpira.
Ilikuwa muda mfupi baada ya Moscow kuinyakua Crimea mnamo 2014 ambapo Sergei na Tatyana Voronkov walipoamua kuondoka Urusi.
Wanandoa hao walikuwa wamekatishwa tamaa kwa muda mrefu na mwelekeo wa nchi yao chini ya utawala wa Rais Vladimir Putin, lakini kunyakuliwa kinyume cha sheria kwa Crimea na kuzuka kwa mapigano mashariki mwa Ukraine kulionekana kuwa hatua ya mabadiliko.
"Tulikuwa tukienda kwenye maandamano [ya kupinga vita], lakini tuligundua haraka kuwa hayakuwa na maana," anasema Sergei, ambaye sasa ana umri wa miaka 55.
"Nilikuwa nikiwaambia marafiki zangu kwamba ni jambo baya kwamba tulikuwa tumechukua Crimea na tulikuwa tukijihusisha na Donbas [eneo kubwa la viwanda mashariki mwa Ukraine]... Walikuwa wakiniambia kwamba ikiwa hatukupenda, tunaweza kuondoka. Kwa hivyo tuliamua kuondoka."
Tatyana, mwenye umri wa miaka 52, ambaye alizaliwa Donbas lakini ni raia wa Urusi kama mumewe, alisema wafanyakazi wenzake ofisini hawakupenda maoni yake dhidi ya Kremlin na aliishia kuacha kazi yake muda mfupi baada ya kunyakuliwa kwa Crimea.

Chanzo cha picha, Family Archive
Kwa miaka mitano iliyofuata, wenzi hao walisafiri kwenda Ukraine kila baada ya miezi sita kutafuta nyumba mpya.
Mnamo mwaka wa 2019, walikaa Novolyubymivka, kijiji cha watu wapatao 300 katika mkoa wa Zaporizhzhia kusini mashariki mwa nchi, ambapo walifuga ng'ombe. Sergei pia alipata kazi kama mpimaji ardhi katzi ambayo alikuwa anaifanya wakati wa utumishi wake katika jeshi la Muungano wa Usovieti.
Mnamo Februari 24, 2022, roketi za kwanza za Urusi ziliruka juu ya nyumba yao.
"Asubuhi nilisikia sauti ya filimbi, kitu kikiruka, na nikatoka nje," Tatyana anakumbuka.
"Roketi ilikuwa ikiruka juu ya nyumba. Nilienda mtandaoni kuona kilichotokea na nikapata kwamba kyiv tayari ilikuwa imepigwa mabomu."

Chanzo cha picha, FAMILY ARCHIVES
Mnamo Februari 26, kijiji cha Novolyubymivka, kilichopo karibu kusini mwa mkoa wa Zaporizhzhia, kilikuwa chini ya uvamizi wa Urusi, ingawa mwanzoni wanandoa hao hawakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na vikosi vya uvamizi.
Lakini siku chache baadaye, wakati msafara wa jeshi la Urusi ulipopita karibu na nyumba yao, Tatyana aliamua kuchukua hatua.
Alipoona msafara huo ukipita, Tatyana alikimbilia ndani, akachukua simu yake, na kumwandikia mtu anayemfahamu huko Kyiv, ambaye aliamini alikuwa na mawasiliano katika huduma za usalama za Ukraine.
Rafiki huyu aliwatumia kifaa cha mawasiliano cha chatbot maalum kwenye programu ya ujumbe wa Telegram. Chatbot iliwafahamisha kuwa watawasiliana na mtu aliye na kitambulisho cha kipekee.
Wanandoa hao waliombwa kutoa eneo na maelezo ya mifumo ya vita vya elektroniki na vifaa vya kijeshi walivyoona, hasa mifumo ya makombora na mizinga. Habari hii ilisaidia jeshi la Ukraine kulenga na kuwaangamiza wanajeshi wa Urusi katika mkoa huo kwa kutumia ndege zisizo na rubani na silaha.
"Hatukufikiria ni usaliti," Tatyana anasema, ingawa wote ni raia wa Urusi.
"Itakuwa uhaini ikiwa Urusi ingeshambuliwa na tunafanya kazi na adui. Lakini hakuna mtu aliyeishambulia Urusi. Hii ilikuwa vita dhidi ya uovu."
Wanandoa hao wanasisitiza kuwa habari waliyoitoa kwa jeshi la Ukraine haikusababisha mashambulizi dhidi ya raia au miundombinu ya raia.

Chanzo cha picha, Anadolu Agency via Getty Images
Kwa miezi miwili, Sergei alikusanya na kuratibu taarifa za ujasusi na Tatyana alizisambaza kutoka kwa simu yake, na kufuta athari zote za ujumbe baadaye.
Wanandoa hao waliendelea kuwasiliana na rafiki yao kwa barua huko Kyiv hadi mwisho wa Aprili 2022, wakati Novolyubymivka ilipoteza mtandao wake.
Wakati huo, watu wenye silaha walikuwa wakija kila wakati kijijini, wakiingia na kutafuta mali. Waliivamia Voronkovs mara kadhaa.
Walipoulizwa kwa nini hawakuondoka katika eneo lililokaliwa, wanandoa hao walijibu: "Tungeenda wapi");