window.__reverb = {}; window.__reverb.__reverbLoadedPromise = new Promise((resolve, reject) => { window.__reverb.__resolveReverbLoaded = resolve; window.__reverb.__rejectReverbLoaded = reject; }); window.__reverb.__reverbTimeout = setTimeout(() => { window.__reverb.__rejectReverbLoaded(); }, 5000);

Mkutano wa Chadema Mwanza: Mbowe akana tuhuma za 'kulambishwa asali'

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe- Chadema amekana kile alicho alichokitaja kuwa ni ''kulishwa asali' .

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo hesho majaaliwa

  2. Mkutano wa Chadema: Mbowe akana tuhuma za 'kulambishwa asali'.

    g

    Chanzo cha picha, Chadema/Twitter

    Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe- Chadema amekana kile alicho alichokitaja kuwa ni ''kulishwa asali' .

    Hii ni baada ya kuingia katika mchakato wa maridhiano na Chama tawala CCM.

    Akihutubia maelfu ya wafuasi wa Chadema, Mbowe amekiri kusikitishwa na tuhuma hizo, huku akisema katu hawezi kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu nia yake ya kutaka madhiriano

    Mbowe
    Maelezo ya picha, Mamia walihudhuria mkutano wa Chadema

    Takwa la kuwepo kwa katiba mpya pia limechukua nafasi ya juu katika ajenda ya mkutano mkuu wa chama cha upinzani Chadema uliofanyika hii leo jijini Mwanza.

    Takriban viongozi wote waliopewa nafasi ya kuhutubia hadhira ya maelfu wa wafuasi wa Chadema waliojitokeza katika uwanja Furahisha wamegusia umuhimu wa kuwepo kwa katiba mpya.

    Mwenyekiti wa Chadema kanda ya ziwa Grayson wanzagi amesema kukosekana kwa utawala bora hivi sasa ni zao la kukuosekana kwa katiba mpya.

    Mambo mengine yaliyojitokeza ni pamoja na matumizi sahihi ya ardhi na jinsi wananchi wanavyoweza kunufaika nayo.

    Peter Msingwa, ambae ni Mwenyekiti wa kanda ya Nyasa kupitia Chadema amesema ni aibu kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuzungukwa na Ziwa Victoria huku wakiwa na shida ya maji na matatizo mengine.

  3. Mkutano wa Chadema: Mbowe akana tuhuma za 'kulambishwa asali'.

    g

    Chanzo cha picha, Chadema/Twitter

    Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe- Chadema amekana kile alicho alichokitaja kuwa ni ''kulishwa asali' .

    Hii ni baada ya kuingia katika mchakato wa maridhiano na Chama tawala CCM.

    Akihutubia maelfu ya wafuasi wa Chadema, Mbowe amekiri kusikitishwa na tuhuma hizo, huku akisema katu hawezi kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu nia yake ya kutaka madhiriano

    Mbowe
    Maelezo ya picha, Mamia walihudhuria mkutano wa Chadema

    Takwa la kuwepo kwa katiba mpya pia limechukua nafasi ya juu katika ajenda ya mkutano mkuu wa chama cha upinzani Chadema uliofanyika hii leo jijini Mwanza.

    Takriban viongozi wote waliopewa nafasi ya kuhutubia hadhira ya maelfu wa wafuasi wa Chadema waliojitokeza katika uwanja Furahisha wamegusia umuhimu wa kuwepo kwa katiba mpya.

    Mwenyekiti wa Chadema kanda ya ziwa Grayson wanzagi amesema kukosekana kwa utawala bora hivi sasa ni zao la kukuosekana kwa katiba mpya.

    Mambo mengine yaliyojitokeza ni pamoja na matumizi sahihi ya ardhi na jinsi wananchi wanavyoweza kunufaika nayo.

    Peter Msingwa, ambae ni Mwenyekiti wa kanda ya Nyasa kupitia Chadema amesema ni aibu kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuzungukwa na Ziwa Victoria huku wakiwa na shida ya maji na matatizo mengine.

  4. Ghasia Burkina Faso: Makumi ya wanawake waliotekwa nyara waachiliwa huru

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Picha za televisheni ya taifa zilionyesha za wanawake na watoto waliookolewa Ijumaa

    Vikosi vya usalama nchini Burkinafaso vimewaokoa wanawake 66 na watoto baada ya kutekwa nyara na wanamgambo wa jihadi kaskazini mwa nchi hiyo wiki iliyopita, imeripoti televisheni ya taifa.

    Katika utekejinyara wa watu wengi ambao haukutarajiwa, waathiriwa walichukuliwa wakati walipokuwa wakikusanya chakula katika eneo lililokumbwa na makundi ya uasi.

    Walipatikana katika basi kwenye kituo cha ukaguzi wa usalama yapata kilomita 200 (maili 125) kusini mwa eneo walikochukuliwa.

    Haijafahamika wazi ni akina nani waliowateka.

    Ijumaa usiku, televisheni ilipnyesha picha za watoto na wanawake, baadhi yao wakiwa wamewabeba watoto wachanga mgongoni, wakipanda basi kwenye uwanja wa ndege baada ya kuhutubiwa na afisa wa jeshi.

  5. Kwa picha: Mkutano wa Chadema Mwanza

    Maelfu ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema wameanza kumiminika katika uwanja wa Furahisha uliopo jijini Mwanza nchini Tanzania.

    Huu ndio mkutano wa kwanza kuitishwa na chama hicho, baada ya Rais wa Samia Suluhu Hassan kuruhusu mikutano ya hadharani baada ya marufukju iliyokuwa imewekwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hayati John pombe Magufuli.

    G
    Maelezo ya picha, Kiongozi wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia - Chadema Freeman Mbowe akielekea kwenye eneo la mkutano
    G
    Maelezo ya picha, Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa kwenye pikipiki kwenye mitaa ya mji wa Mwanza ambako mkutano wa kwanza wa Chadema unatarajiwa kuanza
    g
    Maelezo ya picha, Baadhi ya wachuuzi wa Mwanza waliitumia fursa ya mkutano huo kuuza bidhaa zenye nembo ya Chadema kando ya barabara
    Chadema
  6. Habari za hivi punde, Wafuasi wa Chadema wamiminika Mwanza baada kuondolewa kwa marufuku ya mikutano ya kisiasa ya hadhara,

    G

    Maelfu ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema wameanza kumiminika katika uwanja wa Furahisha uliopo jijini Mwanza nchini Tanzania.

    Heka heka za kuelekea katika eneo hilo ambalo ndipo Chadema itakapofanya mkutano wake mkuu wa kwanza zimeanza kushuhudiwa mapema hii leo.

    Baadhi ya wananchi hao wameonekana wakiwa wamepakiana katika usafiri wa pikipiki maafuru boda huku wakipeperusha bendera za chama hicho na wengine wakiwa katika magari.

    Mkutano huu, unatarajiwa kuvutia maelfu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza pamoja na viunga vyake, huku wengine wakitokea mikoani.

    Wataalamu wa masuala ya kisiasa wanakiri kwamba, mkutano wa leo utaibua hisia kali miongoni mwa wananchi hasa ikizingatiwa kwamba, ni mkutano wa hadhara wa kisiasa kufanyika katika kipindi cha takriban saba.

    d

    Kuanza kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa kunafuatia kauli ya rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ya kuruhusu kufanyika kwa mikutano hiyo baada ya kuwepo kwa marufuku ya miaka kadhaa iliyowekwa na mtangulizi wake John Pombe Magufuli.

    Mwanza imewahi kuwa ngome ya upinzani hata hivyo miaka kadhaa iliyopita, upinzani umeonekana kupoteza ushawishi.

    Huenda kuanza kwa vuguvugu hii kukaleta matumaini mapya miongoni mwa wananchi.

    Unaweza pia kusoma:

    • Je siasa za Tanzania zitabadilika kufuatia kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa?
    • Kufunguliwa kwa mikutano ya hadhara ya siasa Tanzania: 'Tumepokea kwa tahadhari' - Wapinzani
  7. Ujasusi wa Uingereza: Mapigano nchini Ukraine yamekwama

    d

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mji wa Soledar nchini Ukraine, wakati ulipochukuliwa na vikosi vya Urusi

    Taarifa ya ujasusi wa Uingereza iliyotolewa Jumamosi, siku ya 332 ya vita, imeelezea hali katika maeneo ya mapigano.

    Haya ndio mambo makuu kwenye taarifa hii:

    • Katika siku za hivi karibuni, makabiliano makali yamefanyika katika maeneo matatu. Kaskazini mashariki, karibu naKremennaya, na Ukraine huenda ilipata mafanikio machache na iliweza kufanikiwa kujilinda dhidi ya mashambulio ya Urusi.
    • Katika eneo la Bakhmut , jeshi la Urusi na vikosi vya mamluki wa Urusi wa Wagner wanaweza kurejesha uwezo wa mapigano katika mji wa Soledar baada ya kutekwa wiki iliyopita na Ukraine;
    • Kusini, katika jimbo la Zaporizhia, pande zote mbili zimeiongeza idadi ya wanajeshi wake wanaofyatua makombora madogo , na kuepuka kushambulia maeneo makubwa.
    • Kwa ujumla, mapigano yamefikia kiwango cha mkwamo, kuna uwezekano halisi wa kusonga mbele kwa jeshi la Urusi katika eneo la Bakhmut.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Vita vya Ukraine: mengi zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine

  8. Dani Alves: Mlinzi wa zamani wa Barcelona afungiwa mahabusu akishukiwa kwa unyanyasaji wa kingono

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Dani Alves alishinda mataji matatu ya ligi na Ligi tatu za Championi wakati alipokuwa akiichezea Barcelona

    Mlinzi wa Brazil Dani Alves anashikiliwa katika kwa muda gerezani huku akisubiri uchunguzi kuhusiana na madai ya unyanyasaji wa kingono yanayomkabili.

    Mlinzi huyo wa Barcelona, mwenye umri wa miaka 39, anadaiwa kumyanyasa mwanamke kwa kumfusa sehemu ya mwili wake kwa namna isiyofaa walipokuwa katika ukumbi wa starehe wa usiku mjini Barcelona mwezi Disemba.

    Alves, ambaye alikana madai hayo, alipelekwa mahabusu na kuhojiwa na jaji mjini Barcelona Ijumaa.

    Klabu yake, ya Mexico Pumas UNAM, ilikatisha mara moja mkataba wa Alves, kufuatia madai hayo.

    "Klabu ilirejelea kusema kuwa haiwezi kuvumilia vitendo vya mmoja wao yeyote, hata awe nani, ambavyo vinakwenda kinyume na maadili ya klabu ," alisema rais wa mchezo wa klabu ya Pumas, Leopoldo Silva.

    "Hatuwezi kuruhusu mwenendo wa mtu mmoja kuharibu falsafa ya kazi yetu, ambayo imekuwa ya mfano wa kuigwa katika kipindi chote cha historia ya klabu."

    Alves aliiichezea Barcelona mara 408 na pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil katika Kombe la Dunia la 2022.

    Polisi wa eneo hilo Mossos d'Esquadra amethibitisha taarifa ya kukamatwa na kufungwa kwa Alves kwa mashirika ya habari ya Reuters na AFP.

  9. Waziri mkuu wa Uingereza apigwa faini kwa kosa la barabarani

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amepiga faini kwa kutovaa mkanda wa gari wakati gari likisafiri wakati alipokuwa akichukua video kwa akili ya mitandao ya kijamii.

    Polisi katika eneo la Lancashire imesema kuwa imempatia mwanaume mwenye umri wa miaka 42kutoka London adhabu ya kulipa faini ya fedha zilizopangwa kisheria kwa ajili ya kosa hilo.

    Ofisi ya waziri mkuu No 10 imesema kuwa Bw Sunak "anakubali kikamilifu kwamba hili lilikuwa ni kosa na aliomba msamaha ", na kuongeza kuwa atalipa faini.

    Wasafiri ambao hupatikana wakiwa hawajavaa mkanda wa gari huku wakati gari lina mkana huo wanaweza kupigwa faini ya ya pauli 100.

    Faini hii inaweza kuongezeka hadi pauni 500 iwapo kesi itapelekwa mahakamani.

    Waziri mkuu alikuwa katika eneo la Lancashire wakati vido yake ilipochukuliwa, wakati alipokuwa akisafiri kupitia eneo la kaskanini mwa England.

    Video ya kunadi awamu ya hivi karibuni ya serikali ya kunadi ‘’usawazishaji’’ wa matumizi ya serikali- ilitumwa kwenye kweney akaunti ya Instagram ya Bw Sunak.

    Hii ni mara ya pili kwa Bw Sunak kupata adhabu ya kulipa faini akiwa serikalini.

    Mwezi Aprili mwaka jana alitozwa faini pamoja na Boris Johnson na mkewake Carrie kwa kuvunja sheria za ‘’lockdown’’- kwa kuhudhuria kusanyiko la sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Waziri mkuu katika Downing Street mwezi Juni, 2020.

  10. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo tarehe 21.01.2023