Una mimba na hujaolewa?Hapa huishi kwa amani

A couple stand on a bridge in Anzali, northern Iran (28 September 2021)

Chanzo cha picha, Getty Images

Nililazimika kutoa mimba ya mtoto wetu. Yalikuwa maamuzi magumu sana katika maisha yangu yote," anasema Mitra, mbunifu wa vitu vya ndani mwenye miaka 27 anayeishi Tehran na mchumba wake.

Mitra na Mohsen ambaye ni daktari mwenye miaka 32, walianza mahusiano yajulikanayo kama "ndoa nyeupe" - aina ya kuishi kati ya mwanaume na mwanamke kwa kukutana kimwili kabla ya ndoa, huku ikiwa ni kinyume na sheria kali za Kiislamu za Iran .

"Mohsen na mimi tulielewa changamoto zilizo mbele yetu mapema lakini hatukuwa na mipango ya kupata mimba wakati huo," Mitra anaongeza.

Lakini tulibadilisha mawazo na kutaka kuwa na mtoto ambaye angepata cheti cha kuzaliwa kisheria.

Licha ya jitihada kubwa tulizofanya ili kulinda mimba hiyo lakini mazingira yaliwasukuma kutoa mimba.

Kifungu cha sheria namba 1167 cha sheria ya raia wa Irani, ambayo inasema kwamba "mtoto aliyezaliwa kwa uzinzi atabaki kuwa wa wazinifu", inamaanisha kuwa wazazi ambao hawajaoana hawana haki ya kumlea kama wenzi na ni mama tu anayeweza kuomba jina lake liorodheshwe kwenye cheti cha kuzaliwa kwa mtoto.

Kwa mtoto, mamlaka huweka rekodi ya siri ya wale waliozaliwa katika hali kama hizo - habari ambayo inaweza kuwazuia kupata kazi fulani baadaye.

Wakati hakuna takwimu rasmi ya mahusiano ya ndoa nyeupe, ndoa hizo zinazidi kuongezeka na zimekuwa mwiba na kusababisha changamoto nyingi.

Na, kwa kushindwa kuzipunguza, maafisa wanatoa angalizo ambalo linawaweka njia panda na kushindwa kujua nini cha kufanya kwa watoto wanaozaliwa na wapenzi ambao hawajaoana.

"Mwisho wa siku, watoto hao watahitaji kupokea vyeti vyao vya kuzaliwa kabla ya kuandikishwa shuleni," hivi karibuni Naibu Waziri wa Masuala ya Vijana Mohammad Mehdi Tondgouyan aliliambia shirika la habari la Ilna, akionya kuwa athari za kutoshughulikia suala hilo zinaweza kuwa kubwa zaidi.

'Hatutakubali'

Japokuwa wanajua suala la watoto wanaotungwa katika ndoa za utaratibu huu, ni wachache kati ya wasomi wa Iran waliozungumza juu ya hilo hadharani.

Mwanaharakati wa zamani wa mageuzi Parvaneh Salahshouri alitoa tahadhari mnamo Septemba iliyopita, alionya kuwa utoaji mimba ndio chaguo pekee kwa wanawake ambao hawajaolewa lakini wanapata ujauzito.

Lakini Bi Salahshouri alikosolewa vikali na shirika la habari la Fars juu ya "madai yake ya msingi".

Ndoa za kawaida nchini Iran zinakabiliwa na changamoto za kiuchumi na mila ngumu kabla ya ndoa , hali inayowasukuma Wairani kuingia katika mahusiano ambayo si rasmi na hayajaidhinishwa kidini.

Taifa hilo limechukua hatua zaidi ya kuhamasisha kizazi kipya kuingia katika vikundi ambavyo vinatoa mikopo isiyo na riba kusaidia gharama za awali za ndoa.

Parvaneh Salahshouri

Chanzo cha picha, Borna News

Maelezo ya picha, Mbunge wa zamani Parvaneh Salahshouri alionya juu ya utoaji mimba kwa wanawake ambao hawajaolewa

Hii ni kama dawa ya kupunguza maumivu tu," anasema Shina mwenye umri wa miaka 31 kutoka mji wa magharibi wa Hamedan.

"Vipi kuhusu kodi za nyumba zinavyokaba shingo");